Friday, September 19, 2014

MBUYU TWITE AFUARAHIA YANGA KUMALIZANA NA FC LUPOPO

 

Na Fadher Kidevu Blog
BEKI Mbuyu Twite,ameushukuru uongozi wa Yanga kwa kufikia makubaliano na timu yake ya zamani ya FC Lupopo kuhusu madai ya fedha za malipo ya usajili wake.

Baada ya malumbano ya muda uongozi wa Yanga ulikutana na viongozi wa Lupopo Alhamisi ya wiki hii na kufikia makubaliano ya kuilipa klabu hiyo dola 15,000, ambazo ni sawa na Mil 24 za Tanzania kwa utaratibu maalumu.


“Najisikia faraja kuona sasa nipo huru na ninaweza kutimiza majuku yangu kwa umakini mkubwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo lengo langu kwa sasa ni kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kwenye ligi kuu pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho Afrika,”amesema Twite.

No comments:

Post a Comment