Friday, September 5, 2014

KOCHA AZAM ATAMBA YANGA HII HAIWEZI KUMFUNGA NGAO YA JAMII

 

Fadha Kidevu Blog
KOCHA wa Azam Joseph Omog, amesema hauwazii mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga kwa sababu wapinzani wake hawana uwezo wa kukifunga kikosi chake kilicho sheheni mafundi msimu huu.

Omog raia wa Cameroon,alisema anauchukulia mchezo huo kawaida sana kwa sababu malengo yake ni kutetea ubingwa wa Tanzania bara msimu huu kama ilivyokuwa msimu uliopita.

“Kuhusu Ngao ya Jamii sioni cha kunifanya nikose usingizi kwa sababu Yanga nitimu dhaifu mbele ya kikosi change ambacho msimu huu kimesheheni wachezaji wengi mafundi na kipigo kwa ni lazima,”amesema Omog.

Mchezo huo umepangwa kufanyika Septemba 14 badala ya 13 iliyopangwa awali kutokana na sababu mbalimbali zilizotolewa na Shirikisho la soka Tanzania TFF.

No comments:

Post a Comment