Fatma
Salum-Maelezo
Serikali imejipanga kutatua tatizo la makazi kwa
watumishi wa umma kwa kujenga nyumba Elfu 10 za gharama nafuu kote nchini.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw.Elius
Mwakalinga wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika miradi mbalimbali
inayotekelezwa na wakala huo jijini Dar es Salaam na Pwani.
Mwakalinga
alisema kuwa mradi huo wa nyumba elfu 10
unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 18 unahusisha nyumba za viongozi na watumishi
wa kawaida wa kada zote.
“Lengo la
kujenga nyumba hizi ni kuwapatia
watumishi wa umma makazi bora jirani na maeneo yao ya kazi ili kuongeza
tija katika utoaji huduma kwa wananchi. Mradi huu utawawezesha kupata nyumba za
kupanga na kununua kwa gharama nafuu”. Alisema Mwakalinga.
Akifafanua zaidi
Mwakalinga alisema kuwa fedha za
kutekeleza mradi huo zinatokana na ruzuku ya serikali pamoja na fedha za TBA
ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam nyumba hizo zimeanza kujengwa kwenye maeneo ya
Bunju, Mbezi Beach, Ada Estate na Masaki na pia eneo la Chalinze mkoani Pwani.
Aidha Kaimu
Mkurugenzi wa Ushauri kutoka TBA Bw. Edwin Nnunduma alisema kuwa ujenzi wa
nyumba hizo unatumia teknolojia ya kisasa inayopunguza gharama na muda wa
kukamilika.
Pia Nnunduma alisema
mpaka sasa ujenzi unaendelea vizuri kwenye mikoa mbalimbali nchini ikiwemo
mikoa mipya ya Katavi, Geita, Simiyu na Njombe.
Naye Meneja wa
Kikosi cha Ujenzi cha TBA Mhandisi Wilfred Dungamu alieleza kuwa kwa sasa
wakala huo unatumia kikosi cha wahandisi wa ndani kilichoanzishwa mwaka 2012 na
mpango huo umesaidia kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zikitumika kuwalipa
wahandisi kutoka makampuni binafsi.
No comments:
Post a Comment