Friday, September 19, 2014

KIVUMBI CHA LIGI KUU TANZANIA BARA NI LEO....YANGA WATAFANYA NINI MORO?


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

PAZIA la ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 linafunguliwa leo kwa mechi sita kupigwa viwanja mbalimbali nchini.
Macho na masikio ya mashabiki wengi wa soka nchini yatanarajia kuwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo Mtibwa Sugar watakuwa nyumbani kuikaribisha Yanga ya Dar es salaam.
Homa ya pambano hilo ni kubwa mjini humo na tayari majina ya Wabrazil wawili, Genilson Santos Santana ‘Jaja’ na Andrey Coutinho yamekuwa gumzo huku jezi zao zikiongoza kuuzwa.
Mechi nyingine leo hii ni baina ya mabingwa watetezi, Azam fc ambao watakuwa uwanja wa nyumbani wa Azam Complex kuchuana na Polisi Morogoro.
Stand United itakuwa uwanja wa nyumbani wa Kambarage mjini Shinyinga kuoneshana kazi na wageni wenzao, Ndanda fc kutoka mkoani Mtwara.
Katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga, wenyeji Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera.
Maafande wa Ruvu Shootings watasaka pointi tatu muhimu mbele ya Tanzania Prisons ‘Wajelajela’ katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani.
Mechi nyingine kali itapigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambapo wenyeji Mbeya City wanaikaribisha JKT Ruvu ya Pwani.

Ligi hiyo itaendelea kwa mechi moja kupigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha Simba sc dhidi ya Coastal Union

No comments:

Post a Comment