Thursday, September 4, 2014

MAXIMO AWAPOZA MASHABIKI YANGA AKIRI TIMU HAIKUCHEZA VIZURI

 

Na Fadha Kidevu Blog
BAADA ya kuibuka na ushindi kiduchu dhidi ya Thika United ya Kenya kocha wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo amekitetea kikosi chake kwa kusema mbinu na mfumo anavyotaka kuvitumia kwenye ligi ndiyo vilivyo changia timu hiyo kuonyesha kiwango cha chini kwenye mchezo wa jana.
Maximo alisema pamoja na matokeo hayo lakini amewataka mashabiki wa timu hiyo kuondoa hofu na kuwaahidi kulimaliza tatizo hilo kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara Septemba 20 mwaka huu.
“Tatizo hili limetokana na mfumo ambao nimekuwa nikiufundisha ili tuweze kuutumia kwenye ligi siyo kitu rahisi kuma watu wanavyo fikiria lakini nitahakikisha tunatumia vizuri siku zilizobaki kabla ya kuanza kwa ligi ili waweze kuushika na kuufanyia kazi vizuri alisema Maximo.
Yanga keshokutwa Jumapili inatarajia kushukatena uwanja wa taifa Dar es Salaam,kupambana na mabingwa wa Kenya Gor Mahia ukiwa ni mchezo wa mwisho wa kirafiki kabla ya kupambana na Azam kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Septemba 14 mwaka huu

No comments:

Post a Comment