Monday, September 8, 2014

AJALI NYINGINE YATOKEA GAIRO MOROGORO NA KUHUSISHA BASI LA AIRBUS

 

 
Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 35 kujeruhiwa Mkoani Morogoro baada ya  basi la Kampuni ya Airbus lililokuwa likitoka Dar es salaam kwenda Mara  kupinduka eneo katika eneo la Daraja la Mkange kati ya Kijiji cha Berega na Kiegeya  wilayani Kilosa  Mkoani hapa majira ya 5 asubuhi.

Habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Faustine Shilogile ameiambia Father Kidevu Blog kuwa ni kweli kuna ajali nae yupo eneo la tukio.
Mara baada ya ajali hiyo, dereva wake aliyetambuliwa kwa jina la Bilal Seif alikimbia kusiko julikana kukwepa mkono wa sheria na sasa Polisi inamsaka.

Taarifa kutoka eneo la tukio na kwaabadhi ya majeruhi zinaarifu kuwa chanzo cha ajali hiyo iliyolikuta basi hilo lenye namba za ujasili T 106AGB  ni mwendo kasi na kutaka kulipita gari lingine mbele yake.
 

No comments:

Post a Comment