Friday, September 19, 2014

TAMASHA LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI KUFANYIKA SEPTEMBA 22-28-2014 MJINI BAGAMOYO.

       

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba), Michael Kadinde. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 
 Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Abraham Bafadhil "Bura".
 Mkuu wa Mafunzo, Gabriel Kiiza.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba), Michael Kadinde (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Tamasha la 33 la taasisi hiyo litakalofanyika kuanzia Septemba 22 hadi 28 mwaka huu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Abraham Fadhil na Mkuu wa Mafunzo, Gabriel Kiiza.

Dotto Mwaibale
TAASISI ya sanaa na utamaduni Bagamoyo (TaSUba) imeandaa tamasha la 33  lenye lengo la kukuza mila na desturi za watanzania.
Katika tamasha hilo kauli mbiu itakuwa sanaa na utamaduni katika kukuza utalii na mgeni rasmi ni Mbunge wa Afrika Mashariki Makongoro Nyerere ambaye atamwakilisha Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Spika wa Bunge hilo Margareth Zziwa .
Akizungumza  Dar es Salaam leo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba), Michael Kadinde alisema tamasha hilo pia lina lengo la kuonyesha sanaa zilizoandaliwa kiutalaam na wanafunzi wa Tasuba.
“Katika tamasha hili pia tuaihamasisha jamii ije ione tofauti ya sanaa iliondaliwa kitaalamu na isiyo kitaalamu kuweka ushindani kati kati ya taasisi yetu na vikundi vingine,”alisema.
Kadinde alisema katika taasisi yao wanafundisha maigizo,ngoma muziki ufundi wa majukwaa,sanaaza ufundina filamu za televisheni.
“Vikundi ambvyo vitashiriki katika tamasha hilo vya ndani ni 143 na vikundi vya nje vitakuwa vitano Kenya watakuwa na fani ya ngoma,Newzealand watakuwa na muziki, Norway, watakuwa na muziki,Newzealand muziki,Ujerumani maigizo na ,na Korea Kusini watakuwa na muziki,”alisema.

No comments:

Post a Comment