Wednesday, September 3, 2014

Mkongo wa Taifa wasaidia kushuka kwa gharama za mawasiliano nchini.


mHANDISHI ANIFA CHINGUMBE
Mhandisi Hanifa Chingembe akielezea  na kuonyesha kwa waandishi wa habari jinsi mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ulivysambaa nchi nzima.
……………………………………………….
(Picha na Hassan Silayo)
 
Frank Mvungi
Serikali imesema Mkongo wa Taifa umesaidia kushuka kwa gharama za  mawasiliano kwa watumiaji wa mwisho nchini kutoka sh.147 kwa dakika mwaka 2009 hadi shilingi 62 kwa dakika mwaka 2013.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mawsiliano Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Bi Prisca amesema kuwa mkongo wa taifa umesaidia pia kushuka kwa gharama za intaneti kutoka shilingi 36,000 hadi shilingi 9000/Gb kufikia mwaka 2013.
“Mkongo wa Taifa umesesaidia kuharakisha usambazaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara”alisisitiza bi Ulomi.
Katika hatua nyingine, Bi Ulomi alisema faida nyingine ya Mkongo ni kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uwezo wa kusafirisha masafa.
Akieleza kuhusu gharama Bi Prisca amesema gharama za maunganisho ya mawasiliano ya simu za mkononi kutoka  kampuni moja kwenda nyingine                (interconnection fees) ambapo sasa gharama imepungua kutoka sh. 115 hadi shilingi 34.92 kwa dakika.
Mkongo wa Taifa umesaidia kuongeza ushirikiano wa kikanda  kati ya nchi za Afrika Mashariki na kati ambapo nchi za Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, Uganda, na Kenya ambapo hali hiyo imeongeza fursa za kibiashara na kukuza uchumi wa nchi.
Kufikia mwaka 2013 makampuni yafuatayo yalikuwa yameunganishwa na mkongo wa Taifa ni TTCL, TIGO, Zantel,  Airtel, Vodacom, Simbanet na infinity.

No comments:

Post a Comment