Monday, September 8, 2014

SI LAZIMA, ILA NI MUHIMU MANJI AKAWAJIBIKA KWA UONGO WAKE...


 Mwenyekiti wa Yanga sc, Yusuf Manji alitangaza kuwa Emmanuel Okwi hatacheza Simba sc kwasasa ana mkataba na klabu ya Jangwani

Na Baraka Mbolembole

 Suala la mshambulizi, Mganda, Emmanuel Okwi limekwisha. Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji imempa ruhusa ya kujiunga na klabu yoyote mchezaji huyo wa timu ya Taif
Wakati, Yusuph Manji alipotoa tamko la kuitaka TFF kutoa adhabu kwa Okwi na klabu ya Simba baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa muda mfupi na timu ya Simba. 
Manji alisema Okwi bado ni mchezaji bado ni mchezaji halali wa Yanga hadi katikati ya mwaka, 2016, huku akisisitiza kuwa klabu yoyote inayomtaka italazimika kulipa ada ya uhamisho, dola za Kimarekani 500, 000.
  Kama taarifa hiyo ingetolewa na kiongozi wa chini labda isingekuwa na maana kwa walio wengi, lakini kutoka kwa mwenyekiti ilichochea kitu kikubwa. Kwanza ni kuhakikisha kama kweli TFF inauwezo wa kusimamia kanuni na sheria zake, kwa maana kama ingebainika ni kweli Simba na Okwi walivunja sheria kila mmoja alitegemea adhabu kulingana na makosa hayo na si ' maamuzi ya busara' kama ilivyozoeleka. 
Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange 'Kaburu' (kushoto) akiwa na Emmanuel Okwi (kulia)

Lakini sivyo, Okwi ni mchezaji huru, hana mkataba na Yanga na alikuwa na uhuru wa kufanya mazungumzo na klabu yoyote kwa kuwa mkataba wake wa awali na Yanga ulikuwa chini ya miezi sita.
 Licha ya Okwi kutokuwa na mkataba na timu ya Yanga, TFF imetoa taarifa kuwa mchezaji huyo anaidai klabu ya Yanga Tsh.160 millioni! Manji alikuwa tayari kupoteza sifa zake kama kiongozi makini?. 
Achana na matukio yaliyopita chini ya uongozi wake. Alimfuta kazi kocha, Tom Saintfiet ndani ya miezi baada ya timu kufungwa mchezo mmoja. Wakati ule, nilisema kwa sababu alifanya hivyo kwa sababu tu aliambiwa na Tom ' yeye ni mfanyabiashara, na si mfanyabiashara wa kimataifa'.
 Tom alikuwa mtu wa pili kumkosoa, Manji hadharani baada ya awali Iman Madega kufanya hivyo wakati akiwa mwenyekiti wa Yanga na Manji akiwa mfadhili. Kama binadamu mwenye mapungufu, Manji pia anaweza kufanya makosa. Lakini makosa yake hayapaswi kufanyika mara kwa mara katika utawala ambao nyuma yake watu wengi wanakuwa na matarajio wa kufanya kinachotakiwa. 
Enzi hizo Okwi (kulia) akiwa Yanga sc

Jambo la busara kwa Manji hivi sasa ni kuitisha mkutano na vyombo vya habari na kuomba samahani kwa upotoshaji aliotoa kuhusu mkataba wa Yanga na Okwi. Kujiuzulu ni jambo la kiungwana, hasa linapotokea jambo linalokugusa moja kwa moja katika utawala wa walio wengi, kusarenda ni kitu ambacho hakihepukiki kwa Manji, vinginevyo ataendelea kuwa kiongozi asiyeaminiwa na wale anaowaongoza kwa kuwa ni mdanganyifu, hivyo anaweza kufanya hivyo katika jambo kubwa zaidi ya hili la Okwi.
  Je, pesa inamaliza matatizo au matatizo yanamaliza pesa? Yanga wanadaiwa na Okwi, na si Yanga kumdai Okwi. Mchezaji huru husajiliwa bure. Baada ya kucheza mechi 13 na kufunga mabao matano, Okwi amecheza zaidi na vifungu vya sheria na kuwazidi ujanja wanasheria wa Yanga tangu wakati ule akitafuta jinsi ya kutoka Tunisia na kuwa huru. Millioni 100+ millioni 160 kuna namna ya wana-Yanga kumchunguza mwenyekiti wao na kupitia upya mikitaba iliyopo. Manji amejitoa ' kafara' katika suala la Okwi, alijivisha ' bomu' asiloweza kutegua.
 Itashangaza kuona suala la Okwi linakosa hata mtu wa kuwajibika.  Upande wangu, Manji ni mtu wa kwanza anayetakiwa kuachia nafasi yake. ' Amechafuka ', Wako wapi wanasheria wa Yanga?. Hoi!, Okwi ameingiza pesa huku akicheza mpira katika vifungu vya sheria. Sasa ni wakati wa wachezaji wazawa kuamka na kujiamini. Usipolipwa miezi mitatu, wamevunja mkataba wako,…..
0714 08 43 08

No comments:

Post a Comment