Friday, September 19, 2014

YANGA KUWAFUATA MTIBWA SUGER MOROGORO HII LEO

 

Na Fadher Kidevu Blog
WASHINDI  wa Ngao ya Jamii msimu wa 2014/2015 timu ya Yanga inaondoka leo asubuhi  kuelekea Morogoro tayari kwa mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya wakata miwa Mtibwa Sugar katika dimba la Jamhuri.

Yanga chini ya Mbrazil Marcio Maximo imepania kuhakaikisha safari hii inavunja mwiko wa kukosa ushindi katika dimba la Jamhuri kwa takribani miaka minne mfululizo, na maandalizi ya mchezo yanakwenda vizuri  na wachezaji wote wapo fiti ispokuwa kiungo Mbrazili Andrey Coutinho.

Aidha Maximo amesema anatambua Mtibwa Sugar wana kikosi kizuri ambacho kimekaa pamoja kwa muda mrefu, baadhi ya wachezaji aliwahi kuwafundisha akiwa kocha wa timu ya Taifa Taifa Stars  Mecky Mexime ambaye kwa sasa ni kocha wa wana Tamtam hao.

 "Natambua ugumu uliopo kwenye mchezo wa Jumamosi lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata ushindi  Mtibwa nitimu nzuri na watakua nyumbani sikuhiyo wakihitaji pointi tatu lakini hata sisi tunakwenda Morogoro kuhakikisha tunavunja mwiko na kurudi na pointi zote tatu”anasema Maximo.

Kuhusu maendeleo ya mchezaji Andrey Coutinho na Jerson Tegete wanaendelea vizuri na mazoezi lakini daktari ameona wabakie jijini Dar es salaam wakiendelea na programu nyingine chini ya usimamizi wa madaktari wa timi huyo

Kikosi cha wachezaji watakaoondoka kesho asubuhi  Makipa ni: Deo Munishi "Dida", Juma Kaseja na Ally Mustafa "Barthez"

Walinzi: Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro"

Viungo: Mbuyu Twite, Omega Seme, Hassan Dilunga, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima na Said Juma "Makapu"


Washambuliaji: Said Bahanuzi, Hussein Javu, Hamis Kizza, Geilson Santos "Jaja", Saimon Msuva na Mrisho Ngasa 

No comments:

Post a Comment