Mfungaji: Neymar (kulia) akishangilia baada ya kuifungia Brazil goli la ushindi dhidi ya Colombia jana usiku.
NEYMAR akiwa nahodha wa Brazil kwa mara ya kwanza amefanikiwa kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Colombia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa mjini Miami.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza tangu Brazil wafanyiwe kitu mbaya na Ujerumani kwa kufungwa mabao 7-1 katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia na 3-0 katika mchezo wa mshindi wa tatu dhidi ya Uholanzi.
Ushindi wa jana ni faraja kubwa kwa kocha Dunga aliyerithi mikoba ya Luiz Felipe Scolari aliyefungashiwa virago baada ya kuvurunda katika fainali za kombe la dunia zilizomalizika mwezi julai mwaka huu nchini Brazil.
Katika mchezo wa jana nyota wa Manchester United , Radamel Falcao alitokea benchi, lakini ni habari njema kwa Lousi van Gaal kwasababu nyota huyo alikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeruhi.
Nahodha mkali: Neymar, alipigwa picha akimuonesha ufundi mbaya wake Juan Zuniga.
Karudi: Radamel Falcao alicheza dakika 15 tu dhidi ya Brazil
Kikosi cha Brazil: Jefferson, Maicon, Miranda, Luiz (Marquinhos, 80), Luis, Gustavo (Fernandinho, 46), Ramires (Elias, 46), Oscar (Everton Ribeiro), Willian (Coutinho, 72), Diego Tardelli (Robinho, 77), Neymar.
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Rafael Cabral, Danilo, Gil, Marcelo, Goulart.
Mfungaji wa goli: Neymar, 82.
Kadi ya njano: Ramires, Luiz GustavoBooked:
Kikosi cha Colombia: Ospina, Zuniga (Mejia, 73), Zapata, Valdes Parra, Armero, Cuadrado, Ramirez (Arias, 46), Sanchez (Ramos, 85), Rodriguez (Falcao, 77), Martinez (Guarin, 65), Gutierrez (Bacca, 64)
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Vargas, Valencia, Aguilar, Ibarbo, Balanta, Ramos, Quintero, Carbonero, Muriel.
Kadi ya njano: Cudrado, Sanchez, Zuniga, Valdes, Gutierrez.
Kadi nyekundu: Cuadrado.
Watazamaji: 73,429
Mwamuzi: Dave Gantar
No comments:
Post a Comment