Friday, September 19, 2014

PHIRI NIPE NAFASI UONE MAMBO YANGU: TAMBWE

 

Na Fadher Kidevu Blog
MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Burundi Amisi Tambwe,amemtaka kocha wa wake Patrick Phiri,kumpa mechi mbili tu ili aweze kurudisha heshima yake aliyoiweka msimu uliopita kwa kufunga mabao 19.

Tambwe amesema katika siku za karibuni amekosa furaha kufuatia kuwekwa benchi baada ya kuwasili wachezaji Emmanuel Okwi na Raphael Kiongera.

“Kama mchezaji wa kimataifa naamini bado ninauwezo mkubwa wa kufunga mabao kama ilivyokuwa msimu uliopita ndiyo maana namuomba kocha anipe mechi angalau mbili ili aweze kuona uwezo wangu,”amesema Tambwe.

Mfungaji huyo bora wa msimu uliopita kwa sasa hana namba kwenye kikosi cha kwanza cha Simba,baada ya kusajiliwa kwa wachezaji Raphaeli Kiongera na Emmanuel Okwi wa Uganda.


“Mambo yamekuwa magumu kwangu hata yale mazuri niliyofanya msimu uliopita hayakumbukwi tena lakini Mungu ndiyo anajua ila namuomba kocha anipe hata mechi mbili za ligi ili nirudishe heshima,”alisema Tambwe.

No comments:

Post a Comment