Tuesday, September 2, 2014

YANGA KUJIPIMA KWA THIKA UNITED YA KENYA UWANJA WA TAIFA

 

Na Fadhar Kidevu  Blog
KOCHA wa Yanga Marcio Maximo,amesema atashusha kikosi kamili kesho wakati timi hiyo itakapokuwa inapambana na Thika United ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa utakao fanyika kwenye uwanja wa taifa kuanzia saa 11:00 jioni.

Maximo amesema amepania kuwaonyesha staili mpya itakayotumiwa na timu hiyo katika Ligi Kuu ya Tanzania bara ambayo inatarajia kuanza kutumia vumbi Septemba 20 mwaka huu.

“Ningependa mashabiki wa Yanga wajitokeze kwa wingi kesho kuja kujionea viwango vya wachezaji na uwezo wa timu kwa ujumla kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara,”alisema Maximo.

Thika United inayoshiriki ligi kuu nchini Kenya tayari imeshawasili nchini majira ya saa 8 mchana na jioni itafanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Viingilio katika mchezo huo ni VIP A Tshs 30,000/=,VIP B & C Tshs 20,000/=,Orange Tshs 10,000/=,Bluu & Kijanni Tshs 5,000/=

No comments:

Post a Comment