Saturday, September 6, 2014

POLISI WAWILI WAUWAWA KATIKA TUKIO LA KUVAMIWA KITUO CHA POLISI USHIROMBO GEITA


Askari wa wawili wa Jeshi la Polisi kituo Kikuu cha Ushirombo kilichopo Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wafefariki huku wengine wawili wakijeruhiwa baada ya kundi la majambazi kuvamia kituo hicho usiku wa kuamkia leo.

Akitoa taarifa za awali Kamishana wa Polisi Oparesheni na Mafunzo, Paulo Chagonja ameutaarifu uma na kusema kuwa tukio hilo la kusikitisha lilitokea majira ya saa tisa usiku baada ya majambazi hayo kuvamia kituoni hapo na kurusha bomu la kutupwa kwa mkono, ambalo liliweza kuwaua askari polisi hao wawili na webngine wawili kujeruhiwa.

Kamishna Chagonja amewataja Askari Polisi hao waliokufa kuwa ni Askari namba G.2615 PC Dastan Kimati  na WP 7106 PC Uria Mwandiga huku waliojeruhiwa ni Askari namba E. 5831 CPL David na H627 PC Mohamed.

"Aidha katika tukio hilo, majambazi hayo yalifanikiwa kuchukua baadhi ya silaha zilizopo kituoni hapo, ambazo idadi yake bado tunaifuatilia", alisema Kamishna Chagonja.

Chagonja ameiambia Father Kidevu Blog kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Esrnest Mangu yuko eneo la tukio tukio akiongozana na timu ya wataalam wa upelelezi na opraresheni kuhakikisha watuhumiwa wa tukio hilo wanakamatwa haraka.

Jeshi la Polisi limewaomba wananchi watulie na kuwaondoa hofu badala yake wananchi wenye taarifa muhimu zitakazosaidia kuwakamata wahalifu hao wafike na kuzitoa ili wazifanyie kazi.

Hili ni tukio la pili la vutuo vya polisi kuvamiwa ambapo mwezi Juni kituo cha Polisi Kimanzichana walivamiwa na kuuwawa askari na silaha kuporwa.

No comments:

Post a Comment