Friday, September 12, 2014

MSIKITI WA MTAMBANI WASHIKA MOTO TENA

 

Ikiwa ni mwezi mmoja kamili umepita tangu moto mkali uliozuka majira ya saa 12:30 jioni wakati wa swala ya Magharibi na kuteketeza msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es salaam leo tena moto huo umezuka msikitini hapo majira ya saa 6:30 mchana wakati waislamu wanaoswali msikiti huo wakianza kuwasili kwa ajili ya Swala ya Ijumaa.

Leo moto huo umewaka na kuteketeza mali kadhaa katika moja ya vyumba vya msikiti huo ambacho kilikuwa kinatumiwa kama kambi na wanafunzi wa kike wa kidato cha nne na kuteketeza magodoro manne, madaftari pamoja na mali zingine.

Chanzo cha motio huo bado hakija bainika kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura.

No comments:

Post a Comment