Friday, September 30, 2011

Eve E akiwasili jijini Nairobi tayari kwashow


Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Eve E akiwasili mapema leo asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta,jijini Nairobi,Kenya akiwa amepokelewa na mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd kutoka Tanzania,Bwana Balozi Kindamba (shoto) na kulia ni mmoja wa wanausalama wa Eve E,Ujio wa Mwanamuziki huyo anaungana na wanamuziki wengine akiwemo Shaggy,Cabo Snoop pamoja na nyota wa Tusker All Stars Peter Msechu,Davis pamoja na Alpha wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye jukwaa
moja hapo kesho (jumamosi) kwenye viwanja vya Carnivo jijini Nairobi ndani ya tamasha la
Tusker All Stars 2011

MAONYESHO YA NNE YA SWAHILI FASHION WEEK YAZINDULIWA RASMI





Mwasisi wa Swahili Fashion Week Mustafa Hassanali (kulia),akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Ghonche Materego baadaya kuzindua rasmi Nembo mpya ya maonesho hayo.
Mwasisi wa Swahili Fashion Week Mustafa Hassanali,akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Ghonche Materego pamojana wadhamini wa maonesho hayo makubwa ya mavazi .

**************************************
*****************


SWAHILI FASHION WEEK SASA YAWA MAONYESHO MAKUBWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
SWAHILI FASHION WEEK KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

Swahili Fashion Week ambayo ni maonyesho makubwa Afrika Mashariki na Kati, yakiwa  mwaka kwenye wake wa nne yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa  tarehe 10, 11 na 12 mwezi wa Novemba 2011 Dar es Salaam, Tanzania.
Swahili Fashion Week 2011 itawaleta pamoja wabunifu 50 wa mavazi na vishaufu kutoka nchi ziongeazo Kiswahili na nchi nyingine mbali mbali kuonesha ubunifu wao wa hali ya juu na kuonesha mitindo mipya ya mavazi.
“Kwa mwaka huu tumekua maradufu kwani tuna jumla ya wabunifu 21 waliobobea kutoka Tanzania, wabunifu 10 wanaochipukia kutoka Tanzania, na waliosalia wanatoka katika nchi mbali mbali duniani na kwa ujumla wao wanakua wabunifu 50, ambao watakao jiunga na watanzania wote kusherehekea miaka 50 ya UHURU wa nchi yetu.” Alisema Mustafa Hassanali, Mwanzilishi wa maonyesho ya Swahili Fashion Week.
Pamoja na kuwa na maonyesho ya ubunifu wa mavazi kutakua na Maonyesho ya Manunuzi ya bidhaa mbali mbali zinazotengenezwa Tanzaniayalioyoanzishwa mwaka 2010, kwa mara nyingine maonyesho haya yatakua kivutio kikuu katika Swahili Fashion Week. Mpaka hivi sasa, maonyesho haya yana washiriki 30 waliojisajili kushiriki, nahii inafanya maonyesho haya kua maonyesho makubwa nchini.
Kama tulivyokua wa kwanza kuanzisha Maonyesho ya mavazi kama haya, kwa mara nyingine tena tanakua wa kwanza kuanzisha tuzo katika sekta hii ya ubunifu Afrika ya Mashariki na Kati. Kusheherekea mafanikio yaliyofikiwa katika sekta hii ya ubunifu wa mavazi. Kutakua na Mashindano ya Ubunifu wa Fulana ambayo pia ni ya kwanza, kama njia ya kuwashirikisha vijana na vipaji vyao kama njia ya kukuza sekta hii ya familia hii ya wabunifu.
Pia kuna matukio mbali mbali yanayoandaliwa na na yatafanyika kulekea  kwenye maonyesho haya ya Swahili Fashion Week. Kwa kuanza kutakua na maonyesho ya mavazi jijini Arusha ambayo ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, tarehe 8 mwezi Oktoba 2011 kama njia moja wapo ya kupelekea na kusambaza kazi za ubunifu katika mikoa mingine ya Tanzania.
Swahili Fashion week 2011, itakua inarushwa hewani moja kwa moja kupitia tovuti ya www.swahilifashionweek.com kuwapatia fursa wanahabari wa ubunifu duniani kote na kuwajulisha yanayojiri katika ulimwengu wa ubunifu Afrika Mashariki. Maonyesho haya ya moja kwa moja kutoka Makumbusho ya Taifa yatawapatia fursa Watanzania waishio ughaibuni nafasi ya kuunganika na Watanzania wote katika kusheherekea miaka 50 ya UHURU. 
“Tukiwa na malengo ya kukuza biashara hii ya ubunifu katika ukanda huu, ninapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru washirika wetu wote, waliotudhamini katika miaka iliyopita mpaka wakati huu, na pia tungependa kuchukua fursa hii kuhamasisha makampuni na mashirika mbali mbali kujitokeza na kutuunga mkono kwa kudhamini maonyesho haya ya Swahili Fashion Week” Alimalizia Mustafa.
Swahili Fashion week 2011 imedhaminiwa na Nyumba ya Swahili Fashion Week – Hoteli ya Southern Sun, EATV & East Africa Radio, Precision Air, BASATA (Baraza la Sanaa Taifa), Amarula , Ultimate Security, REDDS Original, Image Masters, Global Outdoor ltd, Vayle Springs ltd, Eventslites, Nipashe, Perfect Machinery ltd, Michuzi blog, PKF Tanzania and 361 Degree.

Nyarandu na Mrema wawapongeza Polisi na TRA Moshi kukamata Sukari.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu( Kulia),Mbunge wa Vunjo Mh Augustine Mrema ( Katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mussa Samisi wakizungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kutazama sukari iliyokamatwa katika maeneo ya mipakani Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya mifuko ya sukari iliyokamatwa ikiwa imehifadhiwa katika ghala la Polisi kituo cha Polisi Himo Mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Kituo cha poliosi Himo Afande Majura( Kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalanmdu na Mbunge wa Vunjo Mh Mrema baadhi ya magari yaliyokamatwa yakiwa na bidhaa mbali mbali za magendo ikiwemo sukari.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu( Kushoto), akijibu hoja mbali mbali za Mbunge wa Vunjo Mh Augustino Mrema (Kulia) alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Masoko na vituo vya biashara mipakani kastika Mkoa wa Kilimanjaro. Wanaoshuhudia ni viongozi na watendaji wa Mamlaka mbali mbali katika Mji Mdogo wa Himo.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu akitoa maagizo kwa watendaji wa mamlaka mbali za serikali katika Mji mdogo wa Himo mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea na kukagua masoko na vituo vya Biashara mipakani katika Mkoa wa Kilimanjaro

Kawambwa awataka wahadhiri kuacha kuhubiri siasa Vyuoni


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk, Shukuru Kawambwa, amewataka waadhiri wa vyuo mbalimbali hapa nchini, kuacha tabia ya kuwahubiria siasa wanafunzi wawapo madarasani ukiwa ni muda wa masomo.

Waziri Kawambwa aliyasema hayo jana wakati akizungumza viongizi wa serikali ya wanafunzi, wafanyakazi na uongozi wa chuo Kikuu kishiriki na Biashara cha mjini Moshi (MUCCoBS) wakati alipofanya ziara yake chuoni hapo, na kubainisha kuwa siasa vyuoni haina faida yeyote kwa wanafunzi.

Alisema kuwa baadhi ya waadhiri vyuoni wamekuwa wakibadilisha uwanja wa masomo kuwa jukwaa la kuhubiria siasa kwa wanafunzi, hali iliyosababisha kutokuwepo kwa amani na kuleta machafuko kati ya wanafunzi na serikali.

Waziri Kawamwa alibainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumika na baadhi ya vyama kuwarubuni wanafunzi kujiingiza katika harakati za kisiasa, jambo alilodai wamekuwa wakitumika vibaya bila kutambua hakuna faida yeyote wanayonufaika nayo.

“Wanafunzi wamekuwa wakitumika vibaya kutokana na baadhi ya wahadhiri kutumika na vingozi wa kisiasa kufundisha maswala ya kisiasa darasani. Halii hii inapoteza muda wa kipindi na kwamba wanapojiingiza kwenye maandamano hakuna faida yeyote wanayoipata.” alisema Waziri Kawambwa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WA SWEDEN


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, wakati alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo jijini Stockholm Sweden juzi.
Makamu wa Rais , Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya picha yenye Taswara ya mjini wa Zanzibar, Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, wakati Makamu alipofika Ofisini kwa waziri huyo jijini Stockholm Sweden kwa mazungumzo juzi.

Tamasha la Kilimajaro Bia hilooo



 KILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BONGO 5 MEDIA ZAWAKUTANISHA WASANII WATAKAOTUMBUIZA  KATIKA TAMASHA  LA BIA TANZANIA

Dar es Salaam Septemba 29, 2011- Wasanii zaidi ya kumi watakaotumbuiza katika Tamasha la kwanza la Bia Tanzania Jumamosi na Jumapili katika Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam wameahidi kutoa burudani ya aina yake kwa watanzania.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wasanii hao na wawakilishi waliishukuru Bia ya Kilimanjaro Premium Lager na Kampuni ya Bongo 5 kwa kuandaa tamasha hili kubwa la kwanza na la aina yake Mkoani Dar es salaam,  .

Baadhi ya wasanii na makundi yaliyohudhuria mkutano huo na waandishi wa habari ni Chidi Benz, Msondo Ngoma, Twanga Pepeta, Akudo Impact, Canal top, Tip Top, Ben Paul, Linex, Linah na THT ambao waliwapa wandishi wa habari vionjo kidogo ya vitu ambavyo watavifanya katika tamasha hili.

Kilimanjaro Premium Lager ikishirikiana na Kampuni ya Bongo 5, Alliance Francaise na Taasisi ya Goethe wanandaa tamasha kubwa la bia la kwanza Tanzania ambalo litafanyika katika Viwanja vya Leaders Octoba 1 na 2 mwaka huu.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Bw. George Kavishe alisema tamasha hili litakalojulikana na Kilimanjaro Beer Festival, litakuwa la kwanza na la aina yake kuwahi kufanyika Dar es salam, Mwaka 2007 tuliandaa tamasha kama hili Mkoani Kilimanjaro na 2008 tulifanya Mkoani Arusha na yalikuwa na mafanikio makubwa, sasa tunafanya Dar es salaam  tukiwa na madhumuni ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru na kuwaleta Watanzania pamoja.

Alisema miongoni mwa waalikwa ni wasanii mbalimbali wa Bongo Movies ambao  watajichanganya na watu na kubadilishana mawazo nao na kucheza mechi ya kirafiki na timu zambalimbali za Veterani.
 Tamasha hilo litaanza saa nne kamili asubuhi na litaendelea kwa siku mbili mfulululizo, hadi usiku na kwamba tiketi zitauzwa Tsh 10,000 kwa siku zote mbili na Tsh 7,000 kwa siku moja.

Bw. Kavishe aliwaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili waburudike na kujivunia mafanikio yao baada ya miaka 50 ya Uhuru.

Kwa upande wake, Mratibu wa Matukio, Olive Nimaga aliishukuru TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa jitihada zake za kuwatambua na kuwathamini wateja wake kwa kukukubali kudhamini tamasha hilo la aina yake.
Baadhi ya wanamuziki na waandaaji wa tamasha hilo wakiwa katika picha ya pamoja hhii leo
“Tunawahakikishia mazingira mazuri na salama wakati wa tamasha hili kwani itakuwa wikiendi yenye burudani mbalimbali,” alisema.

Alisema baadhi ya wasanii watakaotoa burudani ni pamoja na Linah, Linex, Chidi Benz, Godzilla, Offside Trick, Akudo Impact, Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wengineo. “Kutakuwa na nyamachoma na vyakula vingine vya aina mbalimbali.

Wednesday, September 28, 2011

YANGA KIMASOMASO

YANGA  jana imewapa raha mashabiki wake baada ya kuifumua Coastal Union ya 
Tanga kwa mabap 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
 Huo unakuwa ushindi mnono zaidi tangu kuanza kwa ligi hiyo Agosti 20, ukifuatiwa na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Moro United, wiki mbili zilizopita.
 Mghana, Kenneth Asamoh alipachika mabao mawili, huku  Mzambia Davies Mwape, Nurdin Bakari na Shamte Ali, kila mmoja akifunga bao moja.
Kwa ushindi  huo, Yanga imepanda hadi nafasi ya nne baada ya kufikisha pointi 12, hivyo kuwafukuzia mahasimu wao wa jadi, Simba wanaoongoza kwa pointi 18, wakifuatiwa na Azam yenye pointi 15 na Ruvu Shooting inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13.

JK AAGANA NA BALOZI WA JAPAN


Rais Jakaya Kikwete akiagana na Balozi wa Japan anayemaliza muda wake nchini, Hiroshi Nakagawa wakati balozi huyo alipokwenda Ikulu jijini Dar es Salaam jana. (PICHA NA FREDDY MARO)

Ni hapatoshi Carnivore Nairobi Jumamosi hii

 

Tuesday, September 27, 2011

TAMASHA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO HALIWEZI KUFA

.

Na Edgar Nazar, Bagamoyo     
 
          Wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo imeamua kutamka bayana kuwa tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo haliwezi kufa. 
 
Akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo jana, katibu mkuu  Wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Seti Kamuhanda amesema kuwa maonyesho ya tamasha yataendelea kuwepo. 
 
 Amesema kuwa amepokea maelezo kutoka kwa mtendaji mkuu wa Tasuba bw. Juma Bakari kwa kuwa wasanii, mahali pa kufanyia kazi na waandaaji wapo tamasha litadumu daima. 
 
Amesema wizara imeona umuhimu wa utamaduni na kuamua kuingiza mpango huo katika mkukuta hivyo kinachotakiwa sasa ni subira. 
 
 Katibu huyo pia amepongeza jitihada za chuo kuongeza ufanisi hali ambayo inatarajiwa kuwa chuo bora Afrika mashariki kwa ubora uliotukuka. 
 
Baada ya ufunguzi huo kulifuatiwa na maonyesho kutoka kwa wenyeji Tasuba pamoja na kikundi cha sanaa za maonyesho cha kutoka Ukerewe mkoani Mwanza. Maonyesho yanatarajiwa kufungwa
oktoba 1.

Monday, September 26, 2011

Mke wa Rais Kikwete awataka wanafunzi kutojiingiza katika Mapenzi



Na Anna Nkinda – Maelezo
26/09/2011 Wanafunzi nchini wametakiwa kuachana na tabia ya kujiingiza katika mapenzi wakiwa  masomoni kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanahatarisha maisha yao kwa kupata maambukizi ya Virusi vinavyosababisha Ugonjwa wa Ukimwi na ujauzito.
Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Kikwete wakati akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Barbro Johansson iliyopo Luguruni jijini Dar es Salaam kwenye  sherehe za mahafali ya kidato cha nne na cha sita.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwaambia wanafunzi hao kuwa elimu wanayoipata  itafungua maisha yao na ya jamii nzima. Itawapa njia ya kuwa na uwezo kiuchumi, itawajengea uwezo wa kujiamini na  kuweza kupaza sauti zao na kusikika kwani watakuwa na upeo mkubwa wa kuchambua mambo na kutoa maamuzi ya busara katika maisha.
 “Ninafahamu kwamba walimu, wazazi na walezi wamekuwa wakiwausia na kuwapa miongozo katika maisha yenu ya kutafuta elimu. Jambo ambalo ningependa muendelee kulizingatia kwa makini ni kwamba elimu mliyoipata bado ni mwanzo tu, hasa ukizingatia kukua kwa utandawazi.
Siku hizi mabadiliko ni ya haraka mno na yanamgusa kila mtu katika kila nyanja ya maisha. Ni vizuri mkajua kwamba ni wajibu wenu kuendelea kujifunza mbinu mpya za kuyakabili mabadiliko haya”, alisema Mama Kikwete.
Mwenyekiti huyo wa WAMA alimalizia kwa kuwataka wanafunzi hao kuchukua tahadhari dhidi  ya ugonjwa wa Ukimwi kwani elimu waliyonayo  haitakuwa na maana kama wataruhusu kuambukizwa ugonjwa huo na kupata ujauzito ambao utawafanya wakatize masomo yao na hivyo kutotimiza ndoto zao

Airtel announces Country Manager for Rwanda operation


 September 23, 2011, NAIROBI : Airtel today announced the appointment of Marcellin Paluku (above in picture) as Country Manger of the company’s newest acquisition – Rwanda.

Mr. Paluku has over 15 years of experience at leading FMCG and telecom companies – including Coca-Cola and Celtel – and has worked in eight markets across the continent. Prior to this appointment, he was the Commercial Director at Airtel DRC where he played a pivotal role in ensuring that Airtel maintained its leadership position.

Speaking about the new appointment, Mr. Jayant Khosla, CEO Anglophone Africa, Bharti Airtel, said: “Rwanda is a market with great growth potential. As with all our operations, the leadership team in Airtel Rwanda will be made up of passionate and experienced Rwandans who are committed to our goal of providing best-in-class mobile broadband services.”

Earlier this month, Airtel was awarded the license to operate 2G and 3G GSM mobile services in Rwanda, expanding the Company’s footprint in Africa to 17 markets. Rwanda has been ranked amongst the fastest growing telecom markets in Africa with a mobile penetration rate of 38.4% in July 2011.

Airtel plans to invest over USD 100 million in Rwanda over the next three years, creating both direct and indirect job opportunities.

Saturday, September 24, 2011

JK afungua mkutano wa DICOTA 2011 jijini Washington DC


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Watanzani nchini Marekani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Diaspora Council of Tanzania in America (DICOTA) 2011 huko Dulles, Virginia, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Wafadhili toka taasisi mbalimbali za umma na binafsi waliofanikisha DICOTA 2011 wakipozi na Rais Kikwete na Meza kuu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe akiongea kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete kuhutubi hadhira na kufungua rasmi mkutano wa DICOTA 2011
Wageni waalikwa wakifurahia hotuba ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete wakati akifungua mkutano huo.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na wageni mbalimbali katika mkutano huo.
Washiriki mbalimbali wa mkutano huo wakimsikiliza Rais Kikwete.
Rais Kikwete akiimbwa wimbo wa Taifa pamoja na meza kuu
Rais Kikwete akiwapongeza watoto kwa kuimba vyema
Sehemu ya waliohudhuria katika mkutano huo
Rais Kikwete akiwa katika banda la Mfuko wa Maendeleo wa Hassan Maajar Trust Fund
Hapa akiwa katika banda la benki ya CRDB
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa washiriki baada ya kutembelea banda la Nyumba Poa katikati ni Peter Mariki Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyumba Poa
Ujumbe mzito toka NSSF ukiwa mkutanoni

TWANGA PEPETA KUSHAMBULIA TAMASHA LA 30 LA SANAA NA UTAMDUNI BAGAMOYO


Bendi maarufu ya African stars "twanga pepeta" inatarajia kufanya onesho katika tamasha la 30 la sanaa na utamaduni la Bagamoyo siku ya Jumatatu tarehe 26.09.2011 ndani ya ukumbi wa Tasuba  mjini Bagamoyo lifanyikapo tamasha hilo kila mwaka .

Kwa mujibu wa mmoja wa waandaji wa onesho hilo bw.Albert kawogo onesho hilo ni maalumu kwa ajili ya miaka 30 ya tamasha hilo ikiwa sambamba na uadhimishaji wa miaka 50 ya uhuru ambayo katika mkoa wa Pwani  inafanyikia mjini  Bagamoyo.

Kawogo aliongeza kuwa onesho hilo la aina yake lilopewa jina la Twanga na Tamasha litakuwa pia linawapa nafasi wakazi wa Bagamoyo na viunga vyake kuzitambua nyimbo mpya za albamu ya Twanga pepeta inayotarajiwa kutambulishwa baadae mwaka huu baada ya albamu ya Mwanadaressalaam.

Onesho hili la kihistoria ndani ya tamasha linafananishwa na onesho lililofanywa kwa mara ya mwisho na iliyokuwa bendi mashuhuri ya Diamond Sound lililofanyika mwaka 2008. Kiingilio katika onesho hili kinatarajiwa kuwa  5000/= na litaanza saa 3:00 usiku.

Ninawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ushuhudia onesho hili la aina yake katika historia ya tamasha alisema Kawogo.

Twanga pepeta inaendelea kutawala tasnia ya muziki wa dansi ikiwa na waimbaji mahiri kama Muumini Mwinjuma,Charles Baba,Luiza Mbutu na wacheza shoo wakali kama Asha Sharapova, Lilian Internet na Maria Salome.


Friday, September 23, 2011

MAANDALIZI YA SENSA YA MAJARIBIO YAANZA


Mkufunzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Neema Ngure akitoa ufafanuzi  wa fomu za dodoso zitakazotumika kwenye sensa ya majaribio ya watu na makazi 2011 kwa wafanyakazi watakaosimamia zoezi hilo litakalofanyika mwezi ujao katika maeneo mbalimbali nchini wakati wa semina ya mafunzo leo mjini Morogoro.
Wafanyakazi watakaosimamia zoezi la sensa ya majaribio ya watu na makazi 2011 kutoka  maeneo mbalimbali nchini wakifanya mtihani wa kupima uelewa leo mjini Morogoro wakati wa semina ya mafunzo ya usimamizi wa zoezi la sensa litakalohusisha maeneo ya mikoa ya Dar es salaam, Kanda ya ziwa, Kanda ya kati, mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini pamoja na Zanzibar.

WAHARIRI WAPIGWA MSASA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU


Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju akifungua semina ya Wahariri wa Vyombo vya habari nchini iliyolenga kuwafahamisha kuhusu kusaidia kuandika habari juu ya haki za binadamu. Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masuala ya mahusiano ya Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Mathew Mwamu.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou hotuba ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju wakati wa Ufunguzi wa Semina ya siku moja ya wahariri wakuu wa vyombo vya habari (TANZANIA EDITORS' FORUM) iliyofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton jijini Dar es Salaam.
Wahariri Wakuu wa Vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada katika Hoteli ya Double Tree By Hilton jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na Mhariri wa Makala wa Gazeti la Serikali la kila siku (Daily News) Deogratius Mushi.

Watanzania wafanya vyema GFC Afika Kusini


Na Mwandishi Wetu TIMU ya Tanzania inayoshiriki kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya kujibu maswali na kupiga mipira yanayojulikana kama Guinness Mpira Chanagmoto yanayoendelea huko Johannesburg Afrika Kusini, wamefanya kufuru isiyotegemewa baada kuongoza mapaka hatua ya tano hapo juzi. 
Kinyang’anyiro hicho kinachoshirikisha jumla ya washiriki 50, 16 wakiwa ni Watanzania na waliobaki ni washiriki wa Kenya na Uganda, kinaendelea hadi hapo kesho kitakapofikia mwisho wa hatua la nane. 
Mpaka jana kabla ya hatua ya sita timu ya George Lukuba na Freddy Jordan ndio waliokuwa vinara kwa kujinyakulia kiasi kizuri cha pesa. Vijana hao walishinda katika hatua za tatu na nne za kinyang’anyiro hicho wakati Sultan Mohamed na Mansoor Seif walikuwa wapili baada ya kina Lukuba. 
Vijana hao wa Kitanzania ambao walionekana kuyumba katika hatua ya mazoezi yaliyofanyika kwa siku mbili katika studio za kisasa za Q ( Q-Studios) zilizopo huko Kew, mpakani na kitongoji cha Alexandra ambacho ni cha pili kwa kukaliwa na Wazalendo wengi wa asili ya Kiafrika baada ya Soweto kwa jiji la Johannesburg, wamewashangaza waandaazi wa changamoto hiyo ya mpira wa miguu. 
Watanzania hao wamekuwa wepesi kujibu maswali na kupiga mipira na kuwabwaga Waganda ambao walianza kwa mbwembwe nyingi wakati wa mazoezi.
Lukuba amesema wao nia yao ni lushinda kuvuta fuba (pesa) hayo yanayotolewa na watengenezaji wa kinywaji cha Guinness ambacho kinasambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini. 
Vijana hao walifanyiwa usaili wiki mbili zilizopita katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, walipanda ndege kuelekea Johannesburg siku ya Jumanne wiki liyopita. Jumla ya hatua nane zinashindaniwa katika kinyang’anyiro hicho ambacho kina toa dola elfu hamsini kila hatua. 
Lukuba ambaye tuliwasiliana naye moja kwa moja jana alisema ndoto ya washiriki wa Kitanzania ni kuendela kuvuta pesa ili kuubwaga umasikini na kuwatoa nishai wenzao wa Kenya na Uganda ambao wamekuwa wakiwabeza kabla ya mashindano kuanza. 
Changamoto hiyo ya Guinness itaoneshwa na televisheni inayopendwa na watazamaji wengi nchini, ITV kwa wiki nane mfululizo. Washindi wa hatua zote nane watajiunga na wanasoka wannne waliostafu soka katika onyesho ambalo pia litashirikisha watazamaji ambao watatuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu zao za mkononi kujaribu bahati yao ya kuvuta pesa hapo baadaye. 
Wachezaji hao ni Jay Jay Okocha wa Nigeria, Rigobert Song wa Cameroon, Kalusha Bwalya wa Zambia na Mfaransa Marcel Desaily aliyekuwa beki mahiri wa timu ya Chelsea na Ufaransa iliyoshinda kombe la Dubnia mwaka 1998. Desaily kwa sass anaishi Accra, Ghana. Hii imekuwa fursa pekee kwa Watanzania kujiongezea kipato kupitia onyesho hilo. 
Labda habari za kusikitisha ni kuhusu mshiriki mmoja wa Kitanzania Juma Nassoro ambaye anaumwa jipu juu ya paja lake la kushoto ambalo limepasuka na anaendelea vizuri. 
Mshiriki mwingine wa Uganda Daniel Elagon amebanwa na malaria tokea siku ya Jumamosi wakati wa hatua ya mwanzo ambapo kulikuwa na baridi kali jijini Johannesburg. Shindano hili la Guinness limekuwa likifanyika katika nchi za Ghana na Cameroon pia Kenya na Uganda walikuwa washiriki kwa mara ya kwanza mwaka jana na hii ni mara yao ya pili. 
Washiriki hao wanatarajiwa kurejea Dar es Salaam siku ya Jumapili kwa ndege ya shirika la ndege la Afrika Kusini saa moja jioni.

Malinzi Mwenyekiti Mpya BMT


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Emmanuel John Nchimbi (Mb) amemteua Bw. Dionis Malinzi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Aidha pia amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa.
    1. Mhe. Jenister Mhagama (Mb)
    2. Mhe. Mkiwa A. Kimwanga (Mb)
    3. Bw. Jamal Rwambow
    4. Bw. Venance Mwamoto
    5. Bw. Juma Pinto
    6. Dkt. Cyprian Maro
    7. Bw. Kanali Eliot Makafu
    8. Bibi Jeniffer Mmasi
    9. Bw. Ramadhani Dau
    10. Bw. Alex Mgongolwa
    11. Bw. Maulid Kitenge
Wengine ni Wajumbe wa kuteuliwa kutokana na nafasi zao:
Mkurugenzi Mkuu - Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Kamishna wa Elimu - Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Mwakilishi - TAMISEMI
Mkurugenzi wa Michezo – Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mwakilishi - Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wajumbe kutoka Wawakilishi wa Vyama vya Michezo (Makatibu) ni:
CHANETA - Chama cha Netiboli Tanzania
TPC - Tanzania Paralympic Committee
AAT - Automobile Association of Tanzania
TSA - Tanzania Swimming Association
BFT - Boxing Federation of Tanzania
RT - Riadha Tanzania
TFF - Tanzania Football Federation
TBF - Tanzania Basketball Federation
TOC - Tanzania Olympic Committee
TTTA - Tanzania Table Tennis Association
 
Uteuzi huu umefanywa kwa kuzingatia Mamlaka ya Waziri chini ya kifungu cha 3(2) cha nyongeza ya Katiba ya Sheria ya BMT Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake katika Sheria Na. 6 ya mwaka 1971.
Wajumbe hao watalitumikia Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu.
Imetolewa na Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo
22.09.2011

Thursday, September 22, 2011

PINDA AFUNGA KLINIKI YA KANISA TARIME


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifungua kliniki ya mama na mtoto katika kituo cha afya cha kanisa Katoliki jimbo la Musoma cha Masanga wilayani Tarime. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Septemba 21,2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Sister Maria wakati alipowasili kwenye misheni ya Kanisa katoliki ya Masanga wilayni Tarime  akiwa katika ziara ya mkoa wa Pwani Septemba 21,2011.
Wasanii wa Tarime wakicheza ngoma maarufu ya Eritungu wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara katika Misheni ya kanisa Katoliki ya Masanga  akiwa katika zaira ya mkoa wa Mara, Septemba 21,2011.

YANGA ,AZAM SAFI SIMBA YAVUTWA MKIA

Mshambuliaji wa Yanga, Kenneth Asamoah (kushoto) akijaribu kuwatoka mabeki wa Villa Squad wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa jana kwenye Uwanja Azam Chamanzi jijini Dar es Salaam.Yanga ilishinda 3-2. Picha na Jackson Odoyo.
Mwandishi Wetu
MABINGWA watetezi Yanga wamewanyuka Villa Squad pungufu kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Chamazi huku vinara wa ligi Simba wakilazimisha sare ya 3-3 na Toto African jijini Mwanza.Wakati Yanga wakipata ushindi wao wa pili na kufikisha pointi tisa, matajiri wa Chamazi, Azam wenyewe wamesogea hadi nafasi ya pili kwenye msimamo kwa kufikisha pointi 14 na kuisogelea Simba inayoongoza kwa pointi 15 baada ya kupata sare ya tatu katika mechi saba.

Macho ya wengi yalikuwa Uwanja wa Chamazi, ambapo Yanga ilipokuwa na kibarua kizito mbele Villa Squad waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia Nsa Job, lakini mabingwa hao walisawazisha kupitia Haruna Niyonzima na Kenneth Asamoah na Hamis Kiiza waliongeza mabao mengine kabla ya Kigi Luseke kuifungia Villa bao la pili na kufanya matokeo kuwa 3-2.

Azam wenyewe wakiwa ugenini itabidi wamshukuru John Boko kwa kuwafungia bao pekee katika mechi dhidi ya Coastal Union akimalizia penalti yake iliyotemwa na kipa.

Katika mechi ya Yanga dhidi ya Villa, nyota wa kimataifa wa Yanga walilipa fadhila kwa kufunga mabao na kumpunguzia presha kocha wao Sam Timbe aliyepewa mechi tatu za kuhakikisha anapata ushindi.

Mshambuliaji Mwape alikosa bao katika dakika ya tano kwa kushindwa kuunganisha krosi ya Ally Shamte iliyotoka sentimita chache kutoka goli la Villa Squad.

Kenneth Asamoah naye alikosa bao baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Oscar Joshua na kutoka nje, wakati nyota hao wa Yanga wakikosa Nsa Job alitumia vizuri mwanya wa kipa Yaw Berko kutoka kwenye mstali na kuinua mpira juu na kujaa wavuni katika dakika ya 11.

Dakika nne baadaye Niyonzima aliisawazishia Yanga bao kwa mpira wa adhabu ambao aliupiga na kwenda moja kwa moja wavuni na kufanya matokeo kuwa 1-1.Kocha wa Villa Squad, Said Chamosi alimtoa Haruna Shamte katika dakika ya 24 na kumwingiza Evalist Maganga.

US kusaidia wasanii wa Tamasha la Mtemi Milambo wa Tabora

Wasanii wa muziki wa asili walioshiriki Tamasha la tatu ta Mtemi Milambo mwaka huu lililofanyika Julai 8-10,201 katika viwanja vya Uyui sekondari Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe.Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila ya Kisukuma na Kinyamwezi.
Wasanii waliofanya vizuri mwaka huu Ali Mango, Asha Kaombwe,Hamis Mpiga, Paulina Muhala, Paul Magadala wataungana na wasanii wengine wa miaka iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa asili iitwayo Mwana Milambo ambayo itakuwa inapiga muziki huo katika mahoteli,maharusi na kumbi mbalimbali za burudani.
 
Nyimbo zitakazorekodiwa ni Kamnyagara kane, Usoga wi kuwa, Kushoke kukaya, kana nabuta, Sensema malunde, Ng,ombe yalala, Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka hamsini ya Uhuru.
 
Lengo kuu ni kuzihifadhi nyimbo mbalimbali zilizotumiwa na wazee wetu wa kale katika vita, kilimo, harusi,na mazishi.
 
Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajiri ya faida ya vizazi vya baadae.
 
Nyimbo hizo zote zitarekodiwa katika studio ya Aegies chini ya muandaaji maarufu Peter John a.k.a Nice P.

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA MIRADI YA MAKAA YA MAWE YA MCHUCHUMA NA CHUMA CHA LIGANGA BAINA YA NDC NA KAMPUNI YA CHINA

 

Makamu wa Rais , Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana  mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Septemba 21, 2011.
Makamu wa Rais , Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Christant Mzindakaya, nje ya ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam leo Septemba 21, baada ya kumalizika kwa zoezi la kutiliana saini mkataba wa ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China.
Makamu wa Rais  Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hngda Corporation Ltd, Liu Canglong, baada ya kuhudhulia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, uliofanyika leo septemba 21 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, baina ya Shirika la maendeleo ya Taifa (NDC) na kamuni hiyo kutoka nchini China.
Makamu wa Rais , Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Bendera maalum ya kumbukumbu ya watu wa China,  wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya (kulia) na  Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, Liu Canglong, (kushoto) waliposainiana mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga katika  ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, jana Septemba 21, 2011.
Makamu wa Rais , Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China, uliofanyika kwenye ukumbu wa Mlimani City Dar es Salaam.
Makamu wa Rais , Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.