Friday, September 2, 2011

NGELEJA AZINDUA KAMATI KAMATI YA KUSIMAMIA MCHAKATO WA UAGIZAJI MAFUTA KWA PAMOJA


Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kushoto), akiwapongeza baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kusimamia mchakato wa uagizaji mafuta wa pamoja, baada ya kuizindua rasmi , Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Charles Sangweni na Tumaini Massaro.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo (kushoto) akisikiliza kwa makini alipokuwa akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja katika hafla hiyo.

Baadhi ya wadau wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kamati ya kusimamia mchakato wa uagizaji mafuta wa pamoja, jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu na Mwenyekiti wa Bodi wa EWURA, Simon Sayore. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA)

Kutoka kulia ni Boss wa EWURA, Haruna Masebu , Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Simon Sayore, Mjumbe wa Bodi ya Ewura, na Mjumbe wa zamani wa Bodi hiyo, Vincent Gondwe
Ngeleja akisalimiana na baadhi ya wajumbe wapya wa Bodi ya Ewura
Waziri Ngeleja akisalimiana na kiongozi wa Umoja wa wauzaji mafuta nchini (TAOMAC), Salum Bisarara. Katikati ni wajumbe wa kamati mpya ya kusimamia mchakato wa uagizaji mafuta kwa pamoja
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kamati ya kusimamia mchakato wa uagizaji mafuta wa pamoja, Dar es Salaam
Waziri Ngeleja akitoka baada ya kuzindua kamati hiyo huku akisindikizwa na kiongozi wa Umoja wa wauzaji mafuta nchini (TAOMAC), Salum Bisarara (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA , Simon Sayore. Uagizaji wa mafuta kwa pamoja unatarajiwa kuanza kabla ya mwaka huu kwisha.

No comments:

Post a Comment