Friday, September 16, 2011

SOKO LA MWANJELWA MBEYA LAUNGUA


Hii ndiyo hali halisi ya moto unaowaka katika soko la Mwanjelwa mjini Mbeya, moto aulioanza asubuhi leo majira ya saa tatu asubuhi, ambapo imedaiwa kwamba moto huo umesababishwa na hitilafu ya mfumo wa umeme katika soko hilo. Inasemekana kuwa hali ni mbaya na uwezekano wa vikosi vya zimamoto kuzima moto huo ni mgumu kutokana na kwamba umeshaenea maeneo mengi ya soko hilo kwani gari mbili zilizokwenda kujaribu kuzima moto huo zimeshindwa, Sokoni hapo kuna vibanda vingi vya wafanyabiashara ndogondogo na maduka ya wafanyabiashara wa kati. Shuhuda wetu ambaye yuko eneo la tukio anasema watu wanakimbia huku na kule ili kuokoa maisha na kuna wengine wanaaguka na kuzirai pia kuna akina mama wawili ambao wamevujika wakati wakikimbia kujiokoa ma moto huo. Taarifa zaidi za madhara ya kibinadamu na hasara ya mali tutawaletea kadiri tutakavyokuwa tukizipata kutoka eneo la tukio.
Moto mkubwa ukiwaka katika soko hilo kama linavyoonekana.
Watu wakihangaika huku na kule ili angalau kuokoa mali zao.
Umati wa watu ukiwa umekusanyika eneo la Mwanjelwa kituo cha mabasi Mwanjelwa.
Watu waengine wakiwa juu ya magari ili kushuhudia tukio hilo ambalo ni la tatu kutokea mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment