Friday, September 30, 2011

Kawambwa awataka wahadhiri kuacha kuhubiri siasa Vyuoni


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk, Shukuru Kawambwa, amewataka waadhiri wa vyuo mbalimbali hapa nchini, kuacha tabia ya kuwahubiria siasa wanafunzi wawapo madarasani ukiwa ni muda wa masomo.

Waziri Kawambwa aliyasema hayo jana wakati akizungumza viongizi wa serikali ya wanafunzi, wafanyakazi na uongozi wa chuo Kikuu kishiriki na Biashara cha mjini Moshi (MUCCoBS) wakati alipofanya ziara yake chuoni hapo, na kubainisha kuwa siasa vyuoni haina faida yeyote kwa wanafunzi.

Alisema kuwa baadhi ya waadhiri vyuoni wamekuwa wakibadilisha uwanja wa masomo kuwa jukwaa la kuhubiria siasa kwa wanafunzi, hali iliyosababisha kutokuwepo kwa amani na kuleta machafuko kati ya wanafunzi na serikali.

Waziri Kawamwa alibainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumika na baadhi ya vyama kuwarubuni wanafunzi kujiingiza katika harakati za kisiasa, jambo alilodai wamekuwa wakitumika vibaya bila kutambua hakuna faida yeyote wanayonufaika nayo.

“Wanafunzi wamekuwa wakitumika vibaya kutokana na baadhi ya wahadhiri kutumika na vingozi wa kisiasa kufundisha maswala ya kisiasa darasani. Halii hii inapoteza muda wa kipindi na kwamba wanapojiingiza kwenye maandamano hakuna faida yeyote wanayoipata.” alisema Waziri Kawambwa.

No comments:

Post a Comment