Wednesday, September 28, 2011

YANGA KIMASOMASO

YANGA  jana imewapa raha mashabiki wake baada ya kuifumua Coastal Union ya 
Tanga kwa mabap 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
 Huo unakuwa ushindi mnono zaidi tangu kuanza kwa ligi hiyo Agosti 20, ukifuatiwa na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Moro United, wiki mbili zilizopita.
 Mghana, Kenneth Asamoh alipachika mabao mawili, huku  Mzambia Davies Mwape, Nurdin Bakari na Shamte Ali, kila mmoja akifunga bao moja.
Kwa ushindi  huo, Yanga imepanda hadi nafasi ya nne baada ya kufikisha pointi 12, hivyo kuwafukuzia mahasimu wao wa jadi, Simba wanaoongoza kwa pointi 18, wakifuatiwa na Azam yenye pointi 15 na Ruvu Shooting inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13.

No comments:

Post a Comment