Monday, September 5, 2011

CHAMI AZINDUA BODI MPYA YA WAKALA WA VIPIMO


Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Cyril Chami (wa pili kutoka kulia), akiwa na baadhi ya wajumbe wapya wa Bidi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), baada ya kuizindua mwishoni mwa wiki, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni, Mjumbe, Paskali Massawe ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha na Rasirimali Watu wa EWURA, Mwenyekiti wa bodi aliyemaliza muda wake, Hosea Kiula, Mwenyekiti mpywa wa Bodi, Rose Lugembe na kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa WMA, Magdalena Chuwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Joyce Mapunjo.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), Hosea Kiula (kulia), akiagana na Mjumbe mpya wa bodi hiyo, Paskali Massawe baada ya hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo kumalizika, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa WMA, Magdalena Chuwa.Massawe ni Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Cyril Chami (wa pili kushoto), akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi aliyemaliza muda wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Cyril Chami (kulia), akiagana na Mjumbe mpya wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), Paskali Massawe baada ya kuzindua bodi hiyo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Massawe ni Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Paskali Massawe ambaye ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Vipimo (WMA), akijitambulisha wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo, uliofanyika mwishoni mwa wiki, Dar es Salaam. Mwenyekiti aliyemaliza muda wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), Hosea Kiula ambaye pia kateuliwa kuwa mjumbe wa bodi hiyo.

Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Paskali Massawe (kushoto) ambaye ni Mjumbe mpya wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa WMA, Magdalena Chuwa baada ya hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo kumalizika, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment