Friday, September 16, 2011

JK AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA MIKOA LEO


 Rais Jakaya Kikwete leo amewaapisha wakuu wapya wa mikoa aliowateua hivi karibu katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Pichani ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Morogoro, JoelNkaya Bendera akipokea nyenzo zake za kufanyia kazi baada ya kula kiapo mbelea ya Rais.
Rais Jakaya, akimwapisha, Saidi Thabiti Mwambungu, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi mamlaka Fatuma Abubakar Mwassa, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Abbas Hussein Kandoro, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Leonidas Tutubert Gama, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza jambo na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati washerehe hizo za kuwaapisha wakuu wapya wa mikoa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wa zamani, Daniel Ole Njoolay (kushoto) akiteta na Mkuu wa mkoa huo wa sasa, Stella Manyanya katika sherehe za kuwaapisha wakuu wa mikoa zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
 Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo za kuwaapisha wakuu wapya wa mikoa.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa walioteuliwa kushika nyadhifa hizo baada ya kuwaapisha katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo

No comments:

Post a Comment