Tuesday, September 20, 2011

WAATHIRIKA WA MABOMU GONGO LA MBOTO WAPEWA FIDIA YA VYOMBO KIDUCHU

Waathirika wa mabomu wa Gongo la Mboto, wakisoma majina ya fidia katika ubao wa matangazo uliopo kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ukonga.

Mke wa Charles Yunusu, Mariam Charles, akiwa mbele ya nyumba yake iliyobomolewa na milipuko ya mabomu katika Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) Gongo la Mboto, akionesha hundi ya malipo ya fidia ya vyombo vyake yenye thamani ya sh.150,000, iliyotolewa Dar es Salaam na Manispaa ya Ilala. Familia hiyo inalalamikia malipo hayo kuwa ni kiduchu na hayalingani na thamani ya mali zilizoteketea.

Mhasibu wa Manispaa ya Ilala, Robin Nabtoel (kushoto), akimkabidhi hundi, Dominica Nchimbi.

No comments:

Post a Comment