Tuesday, September 27, 2011

TAMASHA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO HALIWEZI KUFA

.

Na Edgar Nazar, Bagamoyo     
 
          Wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo imeamua kutamka bayana kuwa tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo haliwezi kufa. 
 
Akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo jana, katibu mkuu  Wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Seti Kamuhanda amesema kuwa maonyesho ya tamasha yataendelea kuwepo. 
 
 Amesema kuwa amepokea maelezo kutoka kwa mtendaji mkuu wa Tasuba bw. Juma Bakari kwa kuwa wasanii, mahali pa kufanyia kazi na waandaaji wapo tamasha litadumu daima. 
 
Amesema wizara imeona umuhimu wa utamaduni na kuamua kuingiza mpango huo katika mkukuta hivyo kinachotakiwa sasa ni subira. 
 
 Katibu huyo pia amepongeza jitihada za chuo kuongeza ufanisi hali ambayo inatarajiwa kuwa chuo bora Afrika mashariki kwa ubora uliotukuka. 
 
Baada ya ufunguzi huo kulifuatiwa na maonyesho kutoka kwa wenyeji Tasuba pamoja na kikundi cha sanaa za maonyesho cha kutoka Ukerewe mkoani Mwanza. Maonyesho yanatarajiwa kufungwa
oktoba 1.

No comments:

Post a Comment